Zaburi 97:1-12
Zaburi 97:1-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA anatawala, nchi na ifurahi, visiwa vyote vishangilie. Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi. Moto hutangulia mbele zake na huteketeza adui zake pande zote. Umeme wake wa radi humulika dunia, nchi huona na kutetemeka. Milima huyeyuka kama nta mbele za BWANA, mbele za Bwana wa dunia yote. Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake. Wote waabuduo sanamu waaibishwa, wale wajisifiao sanamu: mwabuduni yeye, enyi miungu yote! Sayuni husikia na kushangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA. Kwa kuwa wewe, Ee BWANA, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote. Wale wanaompenda BWANA na wauchukie uovu, kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu. Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. Furahini katika BWANA, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu.
Zaburi 97:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu anatawala! Furahi, ee dunia! Furahini enyi visiwa vingi! Mawingu na giza nene vyamzunguka; uadilifu na haki ni msingi wa utawala wake. Moto watangulia mbele yake, na kuwateketeza maadui zake pande zote. Umeme wake wauangaza ulimwengu; dunia yauona na kutetemeka. Milima yayeyuka kama nta mbele ya Mwenyezi-Mungu; naam, mbele ya Bwana wa dunia yote. Mbingu zatangaza uadilifu wake; na mataifa yote yauona utukufu wake. Wote wanaoabudu sanamu wanaaibishwa, naam, wote wanaojisifia miungu duni; miungu yote husujudu mbele zake. Watu wa Siyoni wanafurahi; watu wa Yuda wanashangilia, kwa sababu ya hukumu zako, ee Mungu. Wewe Mwenyezi-Mungu ni mkuu juu ya dunia yote; wewe watukuka juu ya miungu yote. Mwenyezi-Mungu huwapenda wanaochukia uovu, huyalinda maisha ya watu wake; huwaokoa makuchani mwa waovu. Mwanga humwangazia mtu mwadilifu, na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. Furahini kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu; mshukuruni kwa ajili ya jina lake takatifu.
Zaburi 97:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi. Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. Moto hutangulia mbele zake, Nao huwateketeza watesi wake pande zote. Umeme wake uliuangaza ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka. Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA, Mbele za Bwana wa dunia yote. Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake. Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye. Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA. Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya miungu yote. Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru humwangazia mwenye haki, Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo. Enyi wenye haki, mfurahieni BWANA, Na kulishukuru jina lake takatifu.
Zaburi 97:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi. Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. Moto hutangulia mbele zake, Nao huwateketeza watesi wake pande zote. Umeme wake uliuangaza ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka. Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA, Mbele za Bwana wa dunia yote. Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake. Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye. Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA. Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya miungu yote. Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. Nuru imemzukia mwenye haki, Na furaha wanyofu wa moyo. Enyi wenye haki, mmfurahieni BWANA, Na kulishukuru jina lake takatifu.