Zaburi 8:3-6
Zaburi 8:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozisimika huko, mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie, binadamu ni nini hata umjali? Umemfanya awe karibu kama Mungu, umemvika fahari na heshima. Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote; uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake
Zaburi 8:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Zaburi 8:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Zaburi 8:3-6 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji la utukufu na heshima. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.