Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 8

8
Utukufu wa Mungu na cheo cha binadamu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Gitithi. Zaburi ya Daudi)
1Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!
Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu!
2Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao,
umejiwekea ngome dhidi ya adui zako,
uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
3Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota ulizozisimika huko,
4 # Taz Zab 144:3; Ebr 2:6-8 mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,
binadamu ni nini hata umjali?
5Umemfanya awe karibu kama Mungu,
umemvika fahari na heshima.
6 # Taz 1Kor 15:27; Efe 1:22; Ebr 2:8 Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote;
uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake:
7Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini;
8ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.
9Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 8: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha