Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 8

8
Zaburi 8
Utukufu wa Mwenyezi Mungu na heshima ya mwanadamu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!
Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu.
2Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya
umeamuru sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.
3Nikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha,
4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,
binadamu ni nani hata unamjali?
5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,
ukamvika taji la utukufu na heshima.
6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.
7Mifugo na makundi yote pia,
naam, na wanyama wa kondeni,
8ndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kinachoogelea katika njia za bahari.
9Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 8: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia