Zaburi 60:1-12
Zaburi 60:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena. Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika. Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha. Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie. Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme, Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita. Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu? Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
Zaburi 60:1-12 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekuwa na hasira; sasa turejeshe! Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. Umewaonesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni chapeo yangu, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.
Zaburi 60:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, umetutupa na kutuponda, umewaka hasira, tafadhali uturudishie nguvu. Umeitetemesha nchi na kuipasua; uzibe nyufa zake kwani inabomoka. Umewatwika watu wako mateso; tunayumbayumba kama waliolewa divai. Uwape ishara wale wanaokuheshimu, wapate kuuepa mshale. Uwasalimishe hao watu uwapendao; utuokoe kwa mkono wako, na kutusikiliza. Mungu amesema kutoka patakatifu pake “Sasa nitaigawa Shekemu kwa shangwe, Bonde la Sukothi nitalipima sehemusehemu. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, na Yuda ni fimbo yangu ya enzi. Moabu ni kama bakuli langu la kunawia, kiatu changu nitaitupia Edomu kuimiliki. Nitapiga kelele ya ushindi juu ya Filistia.” Ni nani atakayenipeleka kwenye mji wa ngome? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu? Je, umetuacha kabisa, ee Mungu? Wewe huendi tena na majeshi yetu! Utupatie msaada dhidi ya maadui zetu, maana msaada wa binadamu haufai kitu. Mungu akiwa upande wetu tutashinda, yeye atawaponda maadui zetu.
Zaburi 60:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena. Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika. Umewaonesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha. Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli. Ili wapenzi wako waopolewe, Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie. Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nikishangilia. Nitaigawanya Shekemu, Na kulipima bonde la Sukothi. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme, Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita. Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu? Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai kitu. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.