Zaburi 51:1-3
Zaburi 51:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Nihurumie, Ee Mungu, kadiri ya fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa huruma yako. Unioshe kabisa hatia yangu; unisafishe dhambi yangu. Nakiri kabisa makosa yangu, daima naiona waziwazi dhambi yangu.
Zaburi 51:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
Zaburi 51:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Zaburi 51:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.