Zaburi 34:4-7
Zaburi 34:4-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote. Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe. Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote. Malaika wa BWANA huwazungukia, Wamchao na kuwaokoa.
Zaburi 34:4-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilimtafuta BWANA naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. Maskini huyu alimwita BWANA, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote. Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
Zaburi 34:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu, na kuniondoa katika hofu zangu zote. Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Maskini alimlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamsikia, na kumwokoa katika taabu zake zote. Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari.
Zaburi 34:4-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote. Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya. Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote. Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.