Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 34

34
Sifa kwa kukombolewa katika shida
Ya Daudi, alipojifanya mwenye kichaa mbele za Abimeleki, ndipo akafukuzwa na kumtoroka.
1 # 1 Sam 21:13-15 Nitamhimidi BWANA kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2 # Yer 9:24; 1 Kor 1:31 Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie na kufurahi.
3Mtukuzeni BWANA pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4 # Zab 18:6; Yon 2:2; Mt 7:7; Lk 11:9 Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu,
Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.
5Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi,
Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe.
6 # Zab 3:4; 2 Sam 22:1 Maskini huyu aliita, BWANA akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
7 # Dan 6:22; Mwa 32:1; 2 Fal 6:17; Ebr 1:14 Malaika wa BWANA huwazungukia,
Wamchao na kuwaokoa.
8 # 1 Pet 2:3 Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumainia.
9 # Flp 4:19 Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,
Maana, wamchao hawapungukiwi kitu.
10Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
11Njoni, enyi wana, mnisikilize,
Nami nitawafundisha kumcha BWANA.
12 # 1 Pet 3:10-12 Ni nani atamaniye uzima na atakaye kuishi,
Siku nyingi afurahie mema?
13 # 1 Pet 2:22 Uuzuie ulimi wako na mabaya,
Na midomo yako na kusema hila.
14Uache mabaya ukatende mema,
Utafute amani ukaifuatie.
15 # Ayu 36:7 Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake hukielekea kilio chao.
16 # Law 17:10; Yer 44:11; Mit 10:7 Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
17Walilia, naye BWANA akasikia,
Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.
18BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na huwaokoa waliopondeka roho.
19Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini BWANA kutoka kwayo yote.
20 # Yn 19:36 Huihifadhi mifupa yake yote,
Usivunjike hata mmoja.
21 # Zab 94:23 Uovu utamwua asiye haki,
Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
22 # 2 Sam 4:9; Zab 103:4 BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wote wamkimbiliao hawatahukumiwa.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 34: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha