Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 35

35
Sala ya kuponywa kutoka kwa adui
Ya Daudi.
1Ee BWANA, uwapinge hao wanaonipinga,
Upigane nao wanaopigana nami.
2Uishike ngao na kikingio,
Uinuke unisaidie.
3Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia,
Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
4Waaibike na kufedheheka,
Wanaoitafuta nafsi yangu.
Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,
Wanaonizulia mabaya.
5Wawe kama makapi mbele ya upepo,
Malaika wa BWANA akiwaangusha chini.
6Njia yao na iwe giza na utelezi,
Malaika wa BWANA akiwafuatia.
7Maana bila sababu wamenifichia wavu,
Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.
8 # 1 The 5:3; Zab 7:15; Mit 5:22 Uharibifu na umpate kwa ghafla,
Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe;
Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
9 # 1 Sam 2:1; Zab 13:5; Isa 61:10; Ebr 3:18 Na nafsi yangu itamfurahia BWANA,
Na kuushangilia wokovu wake.
10 # Zab 71:19 Mifupa yangu yote itasema,
BWANA, ni nani aliye kama Wewe?
Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye,
Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
11Mashahidi wa udhalimu wanasimama,
Wananiuliza mambo nisiyoyajua.
12Wananilipa mabaya badala ya mema,
Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.
13Bali mimi, walipougua wao,
Nguo yangu ilikuwa gunia.
Nilijitesa nafsi yangu kwa kufunga;
Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
14Nilisikitika kana kwamba ni rafiki au ndugu yangu,
Niliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
15Lakini nikijikwaa wanafurahi na kukusanyana,
Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua,
Wakanipapura bila kukoma.
16Bila heshima walinidhihaki kupindukia,
Wakanisagia meno yao.
17BWANA, utatazama hadi lini?
Uiokoe nafsi yangu kutoka kwa maangamizi yao,
Na maisha yangu kutoka kwa wanasimba.
18Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa;
Nitakusifu kati ya watu wengi.
19 # Zab 69:5; Yn 15:25 Walio adui zangu bure wasinisimange,
Wanaonichukia bila sababu wasining'ong'e.
20Maana hawasemi maneno ya amani,
Ila juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.
21Nao wananifumbulia vinywa vyao,
Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.
22 # Kut 3:7 Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze;
Ee Bwana, usiwe mbali nami.
23Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu
Kwa ajili ya madai yangu,
Mungu wangu na Bwana wangu.
24 # Zab 7:8; 26:1; 2 The 1:6 Unihukumu kwa haki yako,
Ee BWANA, Mungu wangu,
Na usiwaache wanisimange.
25Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo;
Wasiseme, Tumemmeza.
26Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja,
Wanaoifurahia hali yangu mbaya.
Wavikwe aibu na fedheha,
Wanaojikuza juu yangu.
27Washangilie na kufurahi,
Wapendezwao na haki yangu.
Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA,
Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
28Na ulimi wangu utanena haki yako,
Na sifa zako mchana kutwa.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 35: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia