Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 31:1-16

Zaburi 31:1-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa. Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu. Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli. Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini BWANA. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni, Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi. Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu. Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika. Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu. Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

Shirikisha
Soma Zaburi 31

Zaburi 31:1-16 Biblia Habari Njema (BHN)

Kwako, ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama, usiniache niaibike kamwe; kwa uadilifu wako uniokoe. Unitegee sikio, uniokoe haraka! Uwe kwangu mwamba wa usalama, ngome imara ya kuniokoa. Naam, wewe ni mwamba wangu na ngome yangu; kwa hisani yako uniongoze na kunielekeza. Unitoe katika mtego walionitegea mafichoni; maana wewe ni kimbilio la usalama wangu. Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwaminifu. Wawachukia wanaoabudu sanamu batili; lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu. Nitashangilia na kufurahia fadhili zako, maana wewe waiona dhiki yangu, wajua na taabu ya nafsi yangu. Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu; umenisimamisha mahali pa usalama. Unionee huruma, ee Mwenyezi-Mungu, niko taabuni; macho yangu yamechoka kwa huzuni, nimeishiwa nguvu mwilini na rohoni. Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi; naam, miaka yangu kwa kulalamika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka. Nimekuwa dharau kwa maadui zangu wote; kioja kwa majirani zangu. Rafiki zangu waniona kuwa kitisho; wanionapo njiani hunikimbia. Nimesahaulika kama mtu aliyekufa; nimekuwa kama chungu kilichovunjikavunjika. Nasikia watu wakinongonezana, vitisho kila upande; wanakula njama dhidi yangu, wanafanya mipango ya kuniua. Lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu. Nasema: “Wewe ni Mungu wangu!” Maisha yangu yamo mikononi mwako; uniokoe na maadui zangu, niokoe na hao wanaonidhulumu. Uniangalie kwa wema mimi mtumishi wako; uniokoe kwa fadhili zako.

Shirikisha
Soma Zaburi 31

Zaburi 31:1-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ngome thabiti ya kuniokoa. Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze na unichunge. Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu. Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli. Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumainia BWANA. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni, Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama. Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu. Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza. Kwa sababu ya watesi wangu nimelaumiwa, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Wanaoniona njiani wananikimbia. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika. Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu. Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye kutoka kwa adui zangu na wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

Shirikisha
Soma Zaburi 31

Zaburi 31:1-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Nyumba yenye maboma ya kuniokoa. Ndiwe genge langu na ngome yangu; Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu. Mikononi mwako naiweka roho yangu; Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli. Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini BWANA. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni, Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi. Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu. Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika. Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu. Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu. Nyakati zangu zimo mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. Umwangaze mtumishi wako Kwa nuru ya uso wako; Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

Shirikisha
Soma Zaburi 31

Zaburi 31:1-16 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)

Ee Mwenyezi Mungu, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa. Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako. Uniepushe na mtego niliotegewa, maana wewe ndiwe kimbilio langu. Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee Mwenyezi Mungu, uliye Mungu wa kweli. Ninawachukia wale wanaoshikilia sanamu batili; bali mimi ninamtumaini Mwenyezi Mungu. Nitafurahia na kushangilia upendo wako, kwa kuwa uliona mateso yangu na ulijua maumivu ya nafsi yangu. Hukunikabidhi kwa adui yangu bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. Ee Mwenyezi Mungu unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni, nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa. Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na majirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanaoniona barabarani wananikimbia. Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua. Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao. Mwangazie mtumishi wako uso wako, uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.

Shirikisha
Soma Zaburi 31