Zaburi 142:3-6
Zaburi 142:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Ninapokaribia kukata tamaa kabisa, yeye yupo, anajua mwenendo wangu. Maadui wamenitegea mitego njiani mwangu. Nikiangalia upande wa kulia na kungojea, naona hakuna mtu wa kunisaidia; sina tena mahali pa kukimbilia, hakuna mtu anayenijali. Nakulilia wewe, ee Mwenyezi-Mungu! Wewe ni kimbilio langu la usalama; wewe ni riziki yangu kuu katika nchi ya walio hai. Usikilize kilio changu, maana nimekuwa hoi; uniokoe na watesi wangu, maana wamenizidi nguvu.
Zaburi 142:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.
Zaburi 142:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.
Zaburi 142:3-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego. Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. Ee BWANA, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.” Sikiliza kilio changu, kwa sababu mimi ni mhitaji sana; niokoe na wale wanaonifuatilia, kwa kuwa wamenizidi nguvu.