Zaburi 119:70-72
Zaburi 119:70-72 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Mimi nimeifurahia sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
Zaburi 119:70-72 Biblia Habari Njema (BHN)
Mioyo yao imejaa upumbavu, lakini mimi nafurahia sheria yako. Nimefaidika kutokana na taabu yangu, maana imenifanya nijifunze masharti yako. Sheria uliyoweka ni bora kwangu, kuliko mali zote za dunia.
Zaburi 119:70-72 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Lakini mimi nimeifurahia sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa niliteswa, Nipate kujifunza amri zako. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
Zaburi 119:70-72 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako. Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.