Zaburi 105:2-7
Zaburi 105:2-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake. Yeye ndiye BWANA Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote.
Zaburi 105:2-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa; simulieni matendo yake ya ajabu! Jisifieni jina lake takatifu; wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi. Tafuteni msaada kwa Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu; mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima. Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, miujiza yake na hukumu alizotoa, enyi wazawa wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wazawa wa Yakobo, wateule wake; Yeye ndiye Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; hukumu zake zina nguvu duniani kote.
Zaburi 105:2-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Yasimulieni maajabu yake yote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya, Miujiza yake na hukumu alizotoa. Enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Hukumu zake ziko duniani kote.
Zaburi 105:2-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.