Zaburi 105:16-20
Zaburi 105:16-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akasababisha njaa katika nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea. Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. Hadi wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu. Mfalme alituma watu na kumfungua, Mkuu wa watu akamwachilia huru.
Zaburi 105:16-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu alizusha njaa nchini mwao, akaharibu chakula chao chote. Lakini aliwatangulizia mtu mmoja, Yosefu aliyekuwa ameuzwa utumwani. Walimfunga miguu kwa minyororo, na shingoni kwa nira ya chuma, Muda si muda alichotabiri kilitimia. neno la Mwenyezi-Mungu lilimdhibiti. Mfalme wa Misri akaamuru afunguliwe; mtawala wa mataifa akamwachilia huru.
Zaburi 105:16-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea. Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu. Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia.
Zaburi 105:16-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote, naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa. Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma, hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la BWANA lilipomthibitisha. Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru.