Zaburi 105:1-5
Zaburi 105:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
Zaburi 105:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao BWANA na ifurahi. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka
Zaburi 105:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake; yajulisheni mataifa mambo aliyotenda! Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa; simulieni matendo yake ya ajabu! Jisifieni jina lake takatifu; wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi. Tafuteni msaada kwa Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu; mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima. Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, miujiza yake na hukumu alizotoa
Zaburi 105:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Yasimulieni maajabu yake yote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtafuteni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya, Miujiza yake na hukumu alizotoa.