Methali 5:15-23
Methali 5:15-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Hiyo ni yako wewe mwenyewe, wala usiwashirikishe watu wengine. Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa. Mahaba yake yakufurahishe kila wakati, umezwe daima na pendo lake. Mwanangu, ya nini kutekwa na mwanamke mwasherati? Ya nini kumkumbatia kifuani mwanamke mgeni? Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu; yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu. Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe; hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe. Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu, huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.
Methali 5:15-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Matiti yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.
Methali 5:15-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.
Methali 5:15-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe. Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni. Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako. Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake. Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine? Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za BWANA, naye huyapima mapito yake yote. Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu. Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.