Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 5:15-23

Methali 5:15-23 BHN

Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani? Hiyo ni yako wewe mwenyewe, wala usiwashirikishe watu wengine. Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana. Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa. Mahaba yake yakufurahishe kila wakati, umezwe daima na pendo lake. Mwanangu, ya nini kutekwa na mwanamke mwasherati? Ya nini kumkumbatia kifuani mwanamke mgeni? Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu; yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu. Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe; hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe. Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu, huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.

Soma Methali 5