Mit 5:15-23
Mit 5:15-23 SUV
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.