Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 5

5
Maonyo kuhusu unajisi na udanganyifu
1Mwanangu, sikiliza hekima yangu;
Tega sikio lako, uzisikie akili zangu;
2 # Mal 2:7 Upate kuilinda busara,
Na midomo yako iyahifadhi maarifa.
3Maana midomo ya malaya hudondosha asali,
Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 # Mhu 7:26; Ebr 4:12 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;
Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.
5 # Ebr 13:4 Miguu yake inateremkia mauti;
Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;
Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.
7Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,
Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8Itenge njia yako mbali naye,
Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9Usije ukawapa wengine heshima yako,
Na wakatili miaka yako;
10Wageni wasije wakashiba nguvu zako;
Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,
Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
12Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,
Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
13Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,
Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
14Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote,
Katikati ya mkutano na kusanyiko.
15Unywe maji ya tangi lako mwenyewe,
Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
16Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali,
Na mito ya maji katika njia kuu?
17Yawe yako mwenyewe peke yako,
Wala si ya wageni pamoja nawe.
18 # Mhu 9:9; Mal 2:14 Chemchemi yako ibarikiwe;
Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
19 # Wim 2:9 Ni ayala apendaye na paa apendezaye;
Matiti yake yakutoshe sikuzote;
Na kwa upendo wake ushangilie daima.
20Mwanangu! Mbona unashangilia malaya,
Na kukikumbatia kifua cha mgeni?
21 # 2 Nya 16:9; Ayu 31:4; Yer 16:17; Hos 7:2; Ebr 4:13 Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA,
Na mienendo yake yote huitafakari.
22 # Zab 9:15 Maovu yake yeye yatampata mdhalimu,
Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.
23 # Ayu 4:21; Mit 10:21 Atakufa huyo kwa kukosa maonyo,
Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha