Methali 5:1-14
Methali 5:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara, na midomo yako izingatie maarifa. Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu. Yeye haijali njia ya uhai, njia zake ni za kutangatanga, wala hajui. Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu. Iepushe njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakatili miaka yako; wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni. Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu, wala kuwategea sikio wakufunzi wangu. Sasa niko karibu kuangamia kabisa mbali na jumuiya ya watu.”
Methali 5:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
Methali 5:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
Methali 5:1-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine. Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.”