Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 5:1-14

Methali 5:1-14 BHN

Mwanangu, sikia hekima yangu, tega sikio usikilize elimu yangu. Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara, na midomo yako izingatie maarifa. Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali, maneno yake ni laini kuliko mafuta; lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Nyayo zake zaelekea chini mautini, hatua zake zaenda kuzimu. Yeye haijali njia ya uhai, njia zake ni za kutangatanga, wala hajui. Sasa enyi wanangu, nisikilizeni, wala msisahau maneno ya kinywa changu. Iepushe njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakatili miaka yako; wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako, na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni. Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu, wala kuwategea sikio wakufunzi wangu. Sasa niko karibu kuangamia kabisa mbali na jumuiya ya watu.”

Soma Methali 5