Methali 3:18-35
Methali 3:18-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka, na mawingu yakadondosha umande. Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, navyo vitakuwa uhai nafsini mwako, na pambo zuri shingoni mwako. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama, wala mguu wako hautajikwaa. Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu. Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu, Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza; atakuepusha usije ukanaswa mtegoni. Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Usipange maovu dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe bila wasiwasi. Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote. Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake. Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu. Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu. Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha.
Methali 3:18-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande. Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafla, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe. Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote. Usimhusudu mtu mwenye ujeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Methali 3:18-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande. Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe. Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote. Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Methali 3:18-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande. Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako. Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa; ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego. Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote. Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote, kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. Laana ya BWANA i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.