Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 3:18-35

Mithali 3:18-35 SRUV

Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande. Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafla, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe. Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote. Usimhusudu mtu mwenye ujeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.

Soma Mithali 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 3:18-35

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha