Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 3:18-35

Methali 3:18-35 BHN

Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka, na mawingu yakadondosha umande. Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, navyo vitakuwa uhai nafsini mwako, na pambo zuri shingoni mwako. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama, wala mguu wako hautajikwaa. Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu. Usiogope juu ya tishio la ghafla, wala shambulio kutoka kwa waovu, Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza; atakuepusha usije ukanaswa mtegoni. Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Usipange maovu dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe bila wasiwasi. Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote. Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake. Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu. Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu. Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha.

Soma Methali 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Methali 3:18-35

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha