Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 3:18-35

Mithali 3:18-35 NEN

Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande. Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako. Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa; ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego. Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote. Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote, kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. Laana ya BWANA i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 3:18-35

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha