Methali 25:1-13
Methali 25:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho, Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine; Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke. Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
Methali 25:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi nazo ni methali nyingine za mfalme Solomoni walizonakili watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda. Mungu hutukuzwa kwa kuficha mambo, lakini mfalme hutukuzwa kwa yale anayoeleza. Kama zilivyo mbali mbingu na kirefu kina cha ardhi ndivyo zisivyochunguzika akili za mfalme. Toa takataka katika fedha, na mhunzi atakutengenezea chombo kizuri. Waondoe waovu mbele ya mfalme, na utawala wake utaimarika katika haki. Usijipendekeze kwa mfalme, wala usijifanye mtu mkubwa, maana ni heri kuambiwa, “Njoo huku mbele”, kuliko kuporomoshwa mbele ya mkuu. Mambo uliyoyaona kwa macho yako, usiharakishe kuyapeleka mahakamani; maana utafanya nini hapo baadaye, shahidi mwingine akibatilisha hayo usemayo? Suluhisha ugomvi na mwenzako peke yake, na kila mmoja wenu asitoe siri ya mwenzake; watu wasije wakajua kuna siri, ukajiharibia jina lako daima. Neno lisemwalo wakati unaofaa, ni kama nakshi za dhahabu juu ya madini ya fedha. Onyo la mwenye hekima kwa mtu msikivu, ni bora kuliko pete au vito vya dhahabu safi. Mjumbe mwaminifu humfurahisha yule aliyemtuma, kama maji baridi wakati wa joto la mavuno.
Methali 25:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho, Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine; Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke. Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
Methali 25:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho, Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine; Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke. Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
Methali 25:1-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Hizi ni mithali zaidi za Sulemani, zilizonakiliwa na watumishi wa Hezekia mfalme wa Yuda: Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, na ndani yake kutatokea chombo cha mfua fedha. Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha ufalme kitaimarishwa kupitia kwa haki. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha? Ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine, ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha, na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake.