Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 25:1-13

Mithali 25:1-13 NENO

Hizi ni mithali zaidi za Sulemani, zilizonakiliwa na watumishi wa Hezekia mfalme wa Yuda: Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, na ndani yake kutatokea chombo cha mfua fedha. Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha ufalme kitaimarishwa kupitia kwa haki. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha? Ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine, ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha, na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake.