Methali 15:1-4
Methali 15:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kujibu kwa upole hutuliza hasira, lakini neno kali huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini watu wapumbavu hububujika upuuzi. Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya. Ulimi mpole ni chanzo cha uhai, lakini uovu wake huvunja moyo.
Methali 15:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.
Methali 15:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.
Methali 15:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho.