Jawabu la upole hugeuza hasira;
Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri;
Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Macho ya BWANA yako kila mahali;
Yakimchunguza mbaya na mwema.
Ulimi safi ni mti wa uzima;
Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.