Hesabu 6:22-27
Hesabu 6:22-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Mwambie Aroni na wanawe kwamba hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli: Mtawaambia, ‘Mwenyezi-Mungu awabariki na kuwalinda; Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili; Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’ “Ndivyo watakavyotamka jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”
Hesabu 6:22-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabariki wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubariki, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki.
Hesabu 6:22-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.
Hesabu 6:22-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA akamwambia Mose, “Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni: “ ‘ “BWANA akubariki na kukulinda; BWANA akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; BWANA akugeuzie uso wake na kukupa amani.” ’ “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”