Mathayo 22:1-3
Mathayo 22:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano: “Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya harusi. Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje harusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.
Mathayo 22:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mifano, akisema, Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja.
Mathayo 22:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja.
Mathayo 22:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.