Yobu 31:24-32
Yobu 31:24-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu; Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi; Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea katika kung’aa; Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu; Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu. Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu; (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza); Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama? Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu
Yobu 31:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)
“Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu, au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’ Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wangu au kujivunia mapato ya mikono yangu? Kama nimeliangalia jua likiangaza, na mwezi ukipita katika uzuri wake, na moyo wangu ukashawishika kuviabudu, nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake, huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimu maana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu. “Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu, au kufurahi alipopatwa na maafa? La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya, kwa kumlaani ili afe. Watumishi wangu wote wanasema wazi kila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu. Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu, nilimfungulia mlango mpita njia.
Yobu 31:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu; Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu ilikuwa nyingi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi; Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea kung'aa; Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu; Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu. Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu; (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza); Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama? Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu
Yobu 31:24-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata, kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake au mwezi ukienda kwa fahari yake, hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri, au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu, basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa, kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana. “Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu, au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia, lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake; kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema, ‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’ Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani, kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri