Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 31:24-32

Yobu 31:24-32 BHN

“Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu, au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’ Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wangu au kujivunia mapato ya mikono yangu? Kama nimeliangalia jua likiangaza, na mwezi ukipita katika uzuri wake, na moyo wangu ukashawishika kuviabudu, nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake, huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimu maana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu. “Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu, au kufurahi alipopatwa na maafa? La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya, kwa kumlaani ili afe. Watumishi wangu wote wanasema wazi kila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu. Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu, nilimfungulia mlango mpita njia.

Soma Yobu 31