Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 31:24-32

Ayu 31:24-32 SUV

Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu; Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi; Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea katika kung’aa; Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu; Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu. Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu; (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza); Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama? Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu