Yobu 31:1-12
Yobu 31:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nilifanya agano na macho yangu; Basi ningewezaje kumwangalia msichana? Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini, Na urithi wa Mwenyezi utokao juu? Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu? Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote? Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu; (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu); Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku chochote kimeshikamana na mikono yangu; Basi na nipande, mwingine ale; Naam, mazao ya shamba langu na yang'olewe. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu; Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang'oa mavuno yangu yote.
Yobu 31:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nimejifunga rasmi mimi mwenyewe, macho yangu yasimtazame msichana kwa tamaa. Au je, nangojea nini kutoka kwa Mungu aliye juu? Mungu Mwenye Nguvu ameniwekea kitu gani? Je, maafa hayawapati watu waovu na maangamizi wale watendao mabaya? Je, Mungu haoni njia zangu, na kujua hatua zangu zote? “Kama nimeishi kwa kufuata uongo, kama nimekuwa mbioni kudanganya watu, Mungu na anipime katika mizani ya haki, naye ataona kwamba sina hatia. Kama hatua zangu zimepotoka, moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu; kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi, jasho langu na liliwe na mtu mwingine, mazao yangu shambani na yangolewe. “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu, kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu, basi, mke wangu na ampikie mume mwingine, na wanaume wengine wamtumie. Jambo hilo ni kosa kuu la jinai, uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu. Kosa langu lingekuwa kama moto, wa kuniteketeza na kuangamiza, na kuchoma kabisa mapato yangu yote.
Yobu 31:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana? Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini, Na urithi wa Mwenyezi utokao juu? Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu? Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote? Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu; (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu); Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu; Basi na nipande, mwingine ale; Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu; Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang’oa maongeo yangu yote.
Yobu 31:1-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani. Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu, urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu? Je, si uharibifu kwa watu waovu, maangamizi kwa wale watendao mabaya? Je, yeye hazioni njia zangu na kuihesabu kila hatua yangu? “Kama nimeishi katika uongo au mguu wangu umekimbilia udanganyifu, Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, naye atajua kwamba sina hatia: kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, au kama mikono yangu imetiwa unajisi, basi wengine na wale nilichokipanda, nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe. “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu, basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, nao wanaume wengine walale naye. Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa. Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.