Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 31:1-12

Yobu 31:1-12 BHN

“Nimejifunga rasmi mimi mwenyewe, macho yangu yasimtazame msichana kwa tamaa. Au je, nangojea nini kutoka kwa Mungu aliye juu? Mungu Mwenye Nguvu ameniwekea kitu gani? Je, maafa hayawapati watu waovu na maangamizi wale watendao mabaya? Je, Mungu haoni njia zangu, na kujua hatua zangu zote? “Kama nimeishi kwa kufuata uongo, kama nimekuwa mbioni kudanganya watu, Mungu na anipime katika mizani ya haki, naye ataona kwamba sina hatia. Kama hatua zangu zimepotoka, moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu; kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi, jasho langu na liliwe na mtu mwingine, mazao yangu shambani na yangolewe. “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu, kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu, basi, mke wangu na ampikie mume mwingine, na wanaume wengine wamtumie. Jambo hilo ni kosa kuu la jinai, uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu. Kosa langu lingekuwa kama moto, wa kuniteketeza na kuangamiza, na kuchoma kabisa mapato yangu yote.

Soma Yobu 31