Yobu 29:11-25
Yobu 29:11-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba. Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea. Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza. Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake. Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga; Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu; Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu. Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu. Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao. Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika. Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha. Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.
Yobu 29:11-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila aliyesikia habari zangu alinitakia heri na aliponiona, alikubali habari hizo kuwa kweli: Nilimwokoa maskini aliyenililia msaada, kadhalika na yatima asiyekuwa na wa kumsaidia. Waliokuwa karibu kuangamia walinitakia baraka, niliwafanya wajane waone tena furaha moyoni. Uadilifu ulikuwa vazi langu; kutenda haki kulikuwa kama joho na kilemba changu. Kwa vipofu nilikuwa macho ya kuwaonesha njia, kwa viwete nilikuwa miguu yao. Kwa maskini nilikuwa baba yao, nilifanya bidii kutetea haki za watu nisiowajua. Nilizivunja nguvu za watu waovu, nikawafanya wawaachilie mateka wao. Kisha nikafikiri: Nitafia kiotani mwangu nimetulia; siku za maisha yangu zitaongezeka kama mchanga. Mimi ni kama mti uliotandaza mizizi majini, umande wa usiku huburudisha matawi yangu. Napata fahari mpya daima, na nguvu zangu tayari kama mshale na upinde. “Wakati huo watu walinisikiliza na kungoja, walikaa kimya kungojea shauri langu. Nilipomaliza kusema hawakuwa na cha kuongeza, maneno yangu yaliwakolea kama matone ya mvua. Watu waliningojea kama wangojeavyo mvua, walikuwa kama watu wanaotazamia msimu wa vuli. Walipokata tamaa niliwaonesha uso wa furaha, uchangamfu wa uso wangu wakaungangania. Niliwatangulia kuwaongoza, nikawaonesha njia; nilikuwa kwao kama mfalme kati ya majeshi yake; kama mtu anayewafariji wenye msiba.
Yobu 29:11-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. Nilijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba. Nilikuwa macho kwa kipofu, Nilikuwa miguu kwa aliyechechemea. Nilikuwa baba kwa mhitaji, Na kesi ya mtu nisiyemjua niliichunguza. Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake. Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kiota changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga; Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu; Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejeshwa upya mkononi mwangu. Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaza kimya wapate kusikia mashauri yangu. Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao. Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika. Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha. Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.
Yobu 29:11-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, nao walioniona walinisifu, kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia. Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba. Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu. Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete. Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni. Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao. “Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga. Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha. Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’ “Watu walinisikiliza kwa tumaini, wakingojea ushauri wangu kwa utulivu. Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini. Waliningojea kama manyunyu ya mvua na kuyapokea maneno yangu kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli. Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao. Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao; niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake; nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.