Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 29:11-25

Ayubu 29:11-25 SRUV

Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. Nilijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba. Nilikuwa macho kwa kipofu, Nilikuwa miguu kwa aliyechechemea. Nilikuwa baba kwa mhitaji, Na kesi ya mtu nisiyemjua niliichunguza. Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake. Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kiota changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga; Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu; Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejeshwa upya mkononi mwangu. Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaza kimya wapate kusikia mashauri yangu. Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao. Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika. Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha. Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.

Soma Ayubu 29