Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 18:1-21

Yobu 18:1-21 Biblia Habari Njema (BHN)

Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu: “Utawinda maneno ya kusema hadi lini? Tafakari vizuri nasi tutasema. Kwa nini unatufanya kama ng'ombe? Mbona unatuona sisi kuwa wapumbavu? Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au miamba ihamishwe toka mahali pake? “Naam, mwanga wa mtu mwovu utazimishwa; mwali wa moto wake hautangaa. Nyumbani kwake mwanga ni giza, taa inayomwangazia itazimwa. Hatua zake ndefu zitafupishwa; mipango yake itamwangusha chini. Nyayo zake mwenyewe zitamtia mtegoni; kila akitembea anakumbana na shimo. Mtego humkamata kisiginoni, tanzi humbana kabisa. Amefichiwa kitanzi ardhini; ametegewa mtego njiani mwake. Hofu kuu humtisha kila upande, humfuata katika kila hatua yake. Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana; maafa yako tayari kumwangusha. “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake, maradhi ya kifo hula viungo vyake. Anangolewa katika nyumba aliyoitegemea, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho. Nyumba yake tupu, wengine wataishi humo; madini ya kiberiti yametawanywa katika makao yake. Yeye ni kama mti uliokauka mizizi, matawi yake juu yamenyauka. Nchini hakuna atakayemkumbuka; jina lake halitatamkwa tena barabarani. Ameondolewa mwangani akatupwa gizani; amefukuzwa mbali kutoka duniani. Hana watoto wala wajukuu; hakuna aliyesalia katika makao yake. Watu wa magharibi wameshangazwa na yaliyompata, hofu imewakumba watu wa mashariki. Hayo ndio yanayowapata wasiomjali Mungu; hapo ndipo mahali pa wasiomjua Mungu.”

Shirikisha
Soma Yobu 18

Yobu 18:1-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, Je! Hata lini utayawinda maneno kwa mitego? Fikiri, kisha baadaye tutanena. Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani, Tena kuwa wanajisi machoni pako? Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake? Naam, mwanga wa waovu utazimika, Wala muali wa moto wake hautang'aa. Mwanga hemani mwake utakuwa giza, Nayo taa iliyo juu yake itazimwa. Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini. Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi. Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtego utamshika. Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani. Vitisho vitamtia hofu kutoka kila upande, Na kumfukuza karibu na visigino vyake. Nguvu zake zitaliwa na njaa, Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake. Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake. Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho. Katika hema yake hakuna kitakachobaki; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake. Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa. Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani. Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani. Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake, Wala hatasalia mtu hapo alipokaa. Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu. Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu, Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.

Shirikisha
Soma Yobu 18

Yobu 18:1-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, Je! Hata lini utayategea maneno mitambo? Fikiri, kisha baadaye tutanena. Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani, Tena kuwa wanajisi machoni pako? Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake? Naam, mwanga wa waovu utazimika, Wala mwali wa moto wake hautang’aa. Mwanga hemani mwake utakuwa giza, Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa. Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini. Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi. Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtambo utamgwia. Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani. Matisho yatamtia hofu pande zote, Na kumfukuza karibu na visigino vyake. Nguvu zake zitaliwa na njaa, Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake. Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake. Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho. Ambacho si chake kitakaa katika hema yake; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake. Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa. Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani. Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani. Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake, Wala hatasalia mtu hapo alipokaa. Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu. Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu, Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.

Shirikisha
Soma Yobu 18

Yobu 18:1-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Bildadi Mshuhi akajibu: “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea. Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako? Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? “Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika. Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika. Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha. Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu. Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu. Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake. Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua. Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo. Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho. Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake. Mizizi yake chini itakauka na matawi yake juu yatanyauka. Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi. Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, naye amefukuzwa mbali atoke duniani. Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, wala aliyenusurika mahali alipoishi. Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata; watu wa mashariki watapatwa na hofu. Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu; ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”

Shirikisha
Soma Yobu 18