Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 18:1-21

Yobu 18:1-21 BHN

Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu: “Utawinda maneno ya kusema hadi lini? Tafakari vizuri nasi tutasema. Kwa nini unatufanya kama ng'ombe? Mbona unatuona sisi kuwa wapumbavu? Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au miamba ihamishwe toka mahali pake? “Naam, mwanga wa mtu mwovu utazimishwa; mwali wa moto wake hautangaa. Nyumbani kwake mwanga ni giza, taa inayomwangazia itazimwa. Hatua zake ndefu zitafupishwa; mipango yake itamwangusha chini. Nyayo zake mwenyewe zitamtia mtegoni; kila akitembea anakumbana na shimo. Mtego humkamata kisiginoni, tanzi humbana kabisa. Amefichiwa kitanzi ardhini; ametegewa mtego njiani mwake. Hofu kuu humtisha kila upande, humfuata katika kila hatua yake. Alikuwa na nguvu, lakini sasa njaa imembana; maafa yako tayari kumwangusha. “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake, maradhi ya kifo hula viungo vyake. Anangolewa katika nyumba aliyoitegemea, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho. Nyumba yake tupu, wengine wataishi humo; madini ya kiberiti yametawanywa katika makao yake. Yeye ni kama mti uliokauka mizizi, matawi yake juu yamenyauka. Nchini hakuna atakayemkumbuka; jina lake halitatamkwa tena barabarani. Ameondolewa mwangani akatupwa gizani; amefukuzwa mbali kutoka duniani. Hana watoto wala wajukuu; hakuna aliyesalia katika makao yake. Watu wa magharibi wameshangazwa na yaliyompata, hofu imewakumba watu wa mashariki. Hayo ndio yanayowapata wasiomjali Mungu; hapo ndipo mahali pa wasiomjua Mungu.”

Soma Yobu 18