Isaya 62:8-9
Isaya 62:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
Isaya 62:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia, naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema: “Sitawapa tena maadui zako nafaka yako; wala wageni hawatakunywa tena divai yako ambayo umeitolea jasho. Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo, mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu. Nyinyi mliochuma zabibu hizo, mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
Isaya 62:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
Isaya 62:8-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo mmeitaabikia, lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu BWANA, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.”