Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 62

62
1Kwa ajili ya Siyoni sitakaa kimya,
kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,
mpaka kuokolewa kwake kuchomoze kama umeme,
wokovu wake utokeze kama mwenge.
2Mataifa watauona wokovu wako,
wafalme wote watauona utukufu wako.
Nawe utaitwa kwa jina jipya,
jina atakalokupa Mwenyezi-Mungu mwenyewe.
3Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu;
kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.
4Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”,
wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”.
Bali utaitwa: “Namfurahia,”
na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.”
Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe,
naye atakuwa kama mume wa nchi yako.
5Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana,
ndivyo aliyekujenga#62:5 aliyekujenga: Kiebrania: Wanao. atakavyokuwa mume wako.
Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi,
ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako.
6“Juu ya kuta zako ee Yerusalemu nimeweka walinzi,
usiku na mchana kamwe hawatakaa kimya.”
Enyi mnaomkumbusha Mwenyezi-Mungu ahadi yake,
msikae kimya;
7msimpe hata nafasi ya kupumzika,
mpaka atakapousimika mji wa Yerusalemu,
na kuufanya uwe fahari ulimwenguni kote.
8Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia,
naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema:
“Sitawapa tena maadui zako nafaka yako;
wala wageni hawatakunywa tena divai yako
ambayo umeitolea jasho.
9Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo,
mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu.
Nyinyi mliochuma zabibu hizo,
mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
10Wakazi wa Yerusalemu, tokeni, tokeni nje ya mji,
watayarishieni njia watu wenu wanaorejea!
Jengeni! Jengeni barabara na kuondoa mawe yote!
Wekeni alama kwa ajili ya watu.
11 #62:11 Taz Isa 40:10; Ufu 22:12 Mwenyezi-Mungu ametangaza duniani kote,
waambie watu wa Siyoni:
“Mkombozi wenu anakuja,
zawadi yake iko pamoja naye
na tuzo lake liko mbele yake.”
12Nyinyi mtaitwa: “Watu Watakatifu”,
“Watu waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu.”
Na Yerusalemu utaitwa: “Mji aupendao Mungu”,
“Mji ambao Mungu hakuuacha.”

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 62: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia