Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 61

61
Habari njema ya wokovu
1 #61:1-2 Taz Luka 4:18-19 #61:1 Taz Mat 11:5; Luka 7:22Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake,
maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu,#61:1 ameniweka wakfu: Neno kwa neno Kiebrania: Amenipaka mafuta; Taz Orodha ya Maneno chini ya Paka mafuta.
akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema,
niwatibu waliovunjika moyo,
niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru,
na wafungwa kwamba watafunguliwa.
2 #61:2 Taz Mat 5:4 Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema,
na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi;
niwafariji wote wanaoomboleza;
3niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni
taji la maua badala ya majivu,
mafuta ya furaha badala ya maombolezo,
vazi la sifa badala ya moyo mzito.
Nao wataitwa mialoni madhubuti,
aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
4Watayajenga upya magofu ya zamani,
wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza;
wataitengeneza miji iliyobomolewa,
uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.
5Wageni watakuwa hapo kuwachungia mifugo yenu;
watawalimia na kuwatunzia mizabibu yenu.
6Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”,
Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”.
Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa,
mtatukuka kwa mali zao.
7Kwa vile mlipata aibu maradufu,
watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu,
sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu,
na furaha yenu itadumu milele.
8“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki;
nachukia unyanganyi na uhalifu.
Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu,
nitafanya nao agano la milele.
9Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa;
watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine.
Kila atakayewaona atakiri kwamba
wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.”
10 #61:10 Taz Ufu 21:2 Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu,
nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu.
Maana amenivika vazi la wokovu,
amenivalisha vazi la uadilifu,
kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua,
kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake.
11Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea,
na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo,
Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa
kuchomoza mbele ya mataifa yote.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 61: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha