Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 62

62
Uthibitisho wa wokovu wa Sayuni
1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 2#Isa 65:15; Ufu 3:12 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA. 3#Zek 9:16 Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 4#Hos 1:10; 1 Pet 2:10 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba;#62:4 Hefziba: maana yake ni ‘namfurahia.’ na nchi yako Beula;#62:4 Beula: maana yake ni ‘ameolewa.’ kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 5Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
6 # Wim 3:3; Isa 52:8; Eze 3:17; Ebr 13:17 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya; 7#Isa 61:11; Sef 3:20 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapouimarisha Yerusalemu, na kuufanya usifike kote duniani. 8#Kum 28:31; Yer 5:17 BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. 9#Kum 12:12 Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
10Piteni, piteni, katika malango;
Itengenezeni njia ya watu;
Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;
Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.
11 # Zek 9:9; Mt 21:5; Yn 12:15; Isa 40:10; 49:4; Ufu 22:12 Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,
Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, wokovu wako unakuja;
Tazama, thawabu yake iko pamoja naye,
Na malipo yake yako mbele zake.
12Nao watawaita, Watu watakatifu,
Waliokombolewa na BWANA;
Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,
Mji usioachwa.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 62: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia