Isaya 17:1-7
Isaya 17:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa rundo la magofu. Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa mahali pa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu. Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi. Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua na kunona kwa mwili wake kutakwisha. Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai. Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli. Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 17:1-7 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Neno la unabii kuhusu Dameski: “Tazama, Dameski haitakuwa tena mji bali itakuwa lundo la magofu. Miji ya Aroeri itaachwa na itaachiwa mifugo ambayo italala huko, bila yeyote wa kuyaogopesha. Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia, unono wa mwili wake utadhoofika. Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke katika Bonde la Warefai. Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yanayozaa sana,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 17:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kauli ya Mungu dhidi ya Damasko. “Damasko utakoma kuwa mji; utakuwa rundo la magofu. Mitaa yake imeachwa mahame milele. Itakuwa makao ya makundi ya wanyama, wala hakuna mtu atakayewatisha. Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena. “Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa, na unono wake ataupoteza. Atakwisha kama shamba lililovunwa, atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka, atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu. Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni: Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu; nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.” Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli.

Isaya 17:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu. Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu. Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi. Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda. Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai. Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli. Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli.