Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 17

17
Mungu ataadhibu Ashuru na Israeli
1 #17:1-3 Taz Yer 49:23-27; Amo 1:3-5; Zek 9:1 Kauli ya Mungu dhidi ya Damasko.
“Damasko utakoma kuwa mji;
utakuwa rundo la magofu.
2Mitaa yake imeachwa mahame milele.
Itakuwa makao ya makundi ya wanyama,
wala hakuna mtu atakayewatisha.
3Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka,
na utawala wa Damasko utakwisha.
Waashuru ambao watabaki hai,
watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli.
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.
Watakaosalia katika Israeli
4“Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa,
na unono wake ataupoteza.
5Atakwisha kama shamba lililovunwa,
atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka,
atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
6Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni:
Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu;
nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana.#17:6 uzaao sana: Kufuatana na hati ya Kumrani; Kiebrania: Juu ya tawi lake, aliyezaa sana.
Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Mwisho wa kuabudu sanamu
7Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli. 8Hawatazielekea tena madhabahu ambazo ni kazi za mikono yao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, yaani sanamu za mungu Ashera na madhabahu za kufukizia ubani.
9Siku hiyo miji yao imara itaachwa mahame, kama miji ambayo Wahivi na Waamori#17:9 Waamori: Kadiri ya Septuaginta; Kiebrania: Kama magofu ya msitu na kilele cha mlima. waliihama walipokuwa wakiwakimbia wazawa wa Israeli. Kila kitu kitakuwa uharibifu.
10Maana wewe Israeli umemsahau Mungu aliyekuokoa,
hukumkumbuka Mwamba wa usalama wako.
Kwa hiyo, hata mkipanda mimea ya Baali,#17:10 ya Baali: Kiebrania: Ya yule mzuri; labda jina la sifa la Baali.
na kuiweka wakfu kwa mungu wa kigeni;
11hata mkiifanya ikue siku hiyohiyo mliyoipanda
na kuifanya ichanue asubuhi hiyohiyo,
mavuno yenu yatatoweka
siku hiyo ya balaa na maumivu yasiyoponyeka.
Mataifa adui yanashindwa
12Lo! Ngurumo ya watu wengi!
Wananguruma kama bahari.
Lo! Mlio wa watu wa mataifa!
Yanatoa mlio kama wa maji mengi.
13Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi,
lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali.
Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo;
kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
14Wakati wa jioni yanaleta hofu kuu,
lakini kabla ya asubuhi yametoweka!
Hilo ndilo litakalowapata wanaonyakua mali yetu,
ndilo litakalowapata wanaotupora.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 17: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha