Mwanzo 47:7-10
Mwanzo 47:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, Yosefu akamleta baba yake Yakobo kumwamkia Farao; naye Yakobo akampa Farao baraka zake. Farao akamwuliza Yakobo, “Umri wako ni miaka mingapi?” Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.” Kisha Yakobo akambariki Farao, akaondoka.
Mwanzo 47:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao, Yakobo akambariki Farao. Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za kuishi kwako ni ngapi? Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao. Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao.
Mwanzo 47:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao. Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi? Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao. Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao.
Mwanzo 47:7-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Yosefu akamleta Yakobo baba yake na kumtambulisha mbele ya Farao. Baada ya Yakobo kumbariki Farao, Farao akamuuliza, “Je una umri gani?” Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.” Kisha Yakobo akambariki Farao, naye akaondoka mbele ya uso wake.