Kutoka 2:3-4
Kutoka 2:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.
Kutoka 2:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.
Kutoka 2:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini kwa vile hakuweza kumficha zaidi ya muda huo, alitengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipaka namna ya lami, akamtia huyo mtoto ndani. Kisha akakiweka kikapu kando ya mto Nili kwenye majani. Dada yake huyo mtoto akajificha karibu na mahali hapo ili aone yatakayompata nduguye.