Kutoka 2:3-4
Kutoka 2:3-4 BHN
Lakini kwa vile hakuweza kumficha zaidi ya muda huo, alitengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipaka namna ya lami, akamtia huyo mtoto ndani. Kisha akakiweka kikapu kando ya mto Nili kwenye majani. Dada yake huyo mtoto akajificha karibu na mahali hapo ili aone yatakayompata nduguye.