Waefeso 4:2-4
Waefeso 4:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni nyinyi kwa nyinyi kwa mapendo. Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu. Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.
Shirikisha
Soma Waefeso 4Waefeso 4:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Kuna mwili mmoja, na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
Shirikisha
Soma Waefeso 4Waefeso 4:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
Shirikisha
Soma Waefeso 4